Zimbabwe kuweka kando masaibu ya COVID 19

Zimbabwe maarufu kama the Warriors wanashiriki fainali za CHAN kwa mara ya tano wakiwa miongoni mwa nchi tatu zilizoshiriki mara nyingi zaidi.

Zimbabwe inatarajiwa kuweka kando masaibu yaliyokumba safari yao wakielekea Camaroon baada ya wachezaji 9 kuripotiwa kupigwa na homa ya Korona mapema mwezi huu.

Matokeo bora kwa Warriors ni kuibuka ya 4 mwaka 2014 .

Changamoto nyingine waliyo nayo ni kwamba wachezaji wa timu hiyo walipiga mechi kwa mara ya mwisho Novemba 30 mwaka 2019, wakati msimu wa ligi ulipokamilika  ingawa wapo wale wa vilabu vya  FC Platinum na Highlanders walioshiriki mechi za Afrika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka jana kabla ya taifa hilo kuingia katika Lockdown.

Zimbabwe wanafunzwa na mwalimu Zdravko Logarusic aliye na umri wa miaka 54 kutoka Croatia zamani akiinoa Gor Mahia ya Kenya na ana uzoefu baada ya kuifunza timu ya Sudan kwenye fainali za CHAN awali.

The Warriors wanajivunia kipa mwenye tajriba Ariel Sibanda  .

Pambano la ufunguzi kwa Zimbabwe litakuwa  dhidi ya Burkinafasso Jumamosi saa nne usiku.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *