Yanga yampiga teke kocha baada ya siku 37

Miamba wa soka nchini Tanzania kilabu ya Yanga wamemtimua kocha wao Zlatko Krmpotic kutoka Serbia baada ya kuwa usukani kwa siku 37 pekee.

Yanga, walichukua uamuzi wa kumpiga kalamu kocho huyo mapema jumapili siku moja kufuatia ushindi wao wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchuano wa  ligi kuu.

Kocha huyo ambaye awali amezifunza timu za  APR ya Rwanda , Zesco United na  Polokwane City ya Afrika Kusini ndiye meneja wa kwanza kuonyeshwa mlango msimu huu katika ligi kuu ya Tanzania bara.

Chini ya Krmpotic yanga wamecheza mechi 5 kushinda nne na kutoka sare moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *