Wizara ya michezo yakamilisha awamu ya kwanza ya chanjo kwa wanaspoti na wasimamizi wa michezo

Wizara ya michezo imewachanja wanamichezo na maafisa wa michezo jumla ya  4,455  wakipokea chanjo ya covid 19  kote nchini ndani ya siku 12 kufikia Jumatatu  ambayo ilikuwa siku ya mwisho ya shughuli hiyo.

Kulingana na waziri wa michezo Dkt Amina Mohammed watu 4,255 waliopokea chanjo hiyo ya Astra Zenecca ni wa kutoka kaunti ya Nairobi  huku 200 wakitoka kaunti nyinginezo .

Waziri Amina ametoa hakikisho kuwa wanamichezo wote wa timu za taifa ambao walikosa chanjo hiyo watapata hivi karibuni.

Hata hivyo Dkt Amina hajatoa tangazo lolote kuhusu siku wala mipangilio ya kurejelewa kwa michezo nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *