Wizara ya michezo yaanza kuwachanja wachezaji na maafisa 3500

Wizara ya michezo siku ya Alhamisi  imeanzisha mpango wa kuwapa chanjo ya Covid 19 wanamichezo wote nchini  kama njia ya kujiandaa kwa michezo ya olimpiki.

Kulingana na waziri wa michezo Dkt  Amina Mohammed jumla ya wanamichezo 600 walitarajiwa kuchanjwa katika siku ya kwanza,500 Ijumaa na wengine Jumatatu huku jumla ya wanamichezo na wasimamizi wa michezo kwa jumla 3500  wamepokea chanjo hiyo.

“Hatutaki mchezaji yeyote wa Kenya azuiwe kushiriki mashindano kwa sababu ya kukosa kuchanjwa,tunapanga kuanza na wanamichezo wa Olimpiki,wale watakaoshiriki mashindano ya dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 ,maafisa na wanamichezo wa mashindano ya dunia ya Barthes Cup katika raga ,maafisa na washiriki wa mashindano ya world continental tour na wale watakaoshiriki mashindano ya dunia ya Safari Rally ,tunalenga kuwachanja wanamichezo na maafisa 600 leo,Ijumaa 500 na tuendelee hadi mwishoni mwa mwezi huu”

Pia maafisa wote katika wizara ya michezo wanaotangamana na wanamichezo watapewa chanjo hiyo

Shughuli hiyo  itaendelea kote nchini ikiwemo Ngong,kambi ya Eliud Kipchoge na kwa jumla wizara ya michezo ilipokea chanjo 3500 walizotengewa na wizara ya afya.

Hata hivyo kipa umbele  kwa chanjo hiyo itapewa wachezaji na maafisa watakaoshiriki michezo ya Olimpiki ambao wamepiga kambi kwa sasa uwanjani Kasarani.

Waziri amesema kuwa bado kuna mipango ya kufungua michezo nchini  ingawa hawajaafikia uamuzi huo na mazungumzo yanaendelea.

“Kulingana na agizo la Rais michezo bado imefungwa na tutaendelea kuangalia na kujadiliana kuhusu mbinu bora  ya kufungua michezo kwa awamu “akaongeza waziri

Hii ina maana  kuwa michezo mingi nchini huenda ikasubiri kwa muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa kabla ya kufunguliwa tena.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *