Wizara ya Afya yathibitisha visa 1,530 zaidi vya maambukizi ya COVID-19

Wizara ya Afya humu nchini imenakili visa vipya 1,530 vya maambukizi ya virusi vya korona baada ya kupimwa kwa sampuli 8,010 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hii imefikisha idadi jumla ya maambukizi ya virusi hivyo nchini kuwa 132,646 huku jumla ya sampuli zilizopimwa ikifika 1,480,240

Kati ya visa hivyo vipya, 1,468 walikuwa Wakenya huku 62 wakiwa raia wa kigeni.

Visa 842 ni vya wanaume ilhali 688 ni vya wanawake, wote wa kati ya umri wa miezi mitatu hadi miaka 99.

Kaunti ya Nairobi imenakili visa 686, Nakuru 164, Kiambu 151, Kitui 68, Nyeri 67, Uasin Gishu 65, Machakos 41, Kajiado 30, Mombasa 29, Kisumu 26, Nyandarua 24, Embu 24, Busia 23, Makueni 19, Murang’a 16, Nandi 15, Kilifi 15, Taita Taveta 10, Meru 9, Trans Nzoia 8, Laikipia, Kakamega, Pokot Magharibi visa 7 kila moja, Kirinyaga 3, Baringo, Kisii, Turkana, Vihiga visa 2 kila moja, huku Bungoma, Elgeyo Marakwet, Garissa, Isiolo, Kericho, Nyamira, Siaya na Tharaka Nithi zikiripoti kisa kimoja kimoja.

Wagonjwa 129 wamepona kutokana na virusi hivyo, 74 walitoka katika mpango wa kuwashughulikia wagonjwa nyumbani huku 55 wakipona kutoka hospitali mbali mbali nchini. Idadi jumla ya waliopona sasa ni watu 92,290.

Hata hivyo, wagonjwa 12 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kuwa 2,147.

Kwa sasa wagonjwa 1,308 wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini huku wengine 4,760 wakiuguzwa nyumbani.

Kati ya wanaohudumiwa hospitalini, 152 wako katika vitengo vya wagonjwa mahututi, 56 kati yao wakiwa wanatumia mashine za kupumulia na wengine 97 wakipokea hewa ya ziada ya oksijeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *