Wizara ya Afya yatangaza visa vipya 486 vya maambukizi ya korona

Wizara ya Afya humu nchini imethibitisha visa vipya 486 vilivyotokana na upimaji wa sampuli 2,989 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Jumla ya visa vya maambukizi vimefikia watu 146,156 na kuongeza idadi ya waliopimwa kufikia watu 1,564,827.

Kati ya wale waliopimwa 457 ni Wakenya ilhali 29 ni raia wa kigeni, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya. Wanaume walioambukizwa ni 293, huku wanawake wakiwa 193.

Mgonjwa wa umri wa chini zaidi ni mtoto wa umri wa miezi minne na wa umri wa juu ni mtu wa umri wa miaka 94.

Visa hivyo vipya vimenakiliwa katika magatuzi mbali mbali kama ifuatavyo: Nairobi 349, Kiambu 21, Uasin Gishu 21, Mombasa 17, Kilifi 16, Kajiado 14, Machakos 12, Nakuru 11, Kwale 5, Kericho 4, Kirinyaga 2, Kitui 2, Nyeri 2, Mandera 1, Murang’a 1, Samburu 1, Siaya 1, Kisumu 1, Taita Taveta 1, Turkana 1, Bomet 1, Busia 1 na Elgeyo Marakwet 1.

Wagonjwa 115 wamepona, 54 ni kutoka utunzi wa nyumbani na 61 ni kutoka hospitali mbali mbali. Jumla ya waliopona sasa wamefikia 99,210.

Wagonjwa 1,645 kwa wakati huu wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini huku 6,063 wakiwa chini ya utunzi wa nyumbani. Wagonjwa 248 wamelazwa katika wodi za wagonjwa mahututi, 48 kati yao wakiwa wanasaidiwa kupumua na wengine 169 wanapokea hewa ya oksijeni.

Hata hivyo, wagonjwa 20 wameaga dunia na kuongeza jumla ya maafa yaliyotokana na COVID-19 hadi 2,368.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *