William Ruto amtakia Raila Odinga afueni ya haraka

Naibu Rais Dkt. William Ruto amemtumia aliyekuwa Waziri mkuu Raila Odinga, ujumbe wa afueni ya haraka baada ya Odinga kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Covid-19.

Katika ujumbe huo, Ruto alielezea imani kwamba Odinga atashinda vita dhidi ya maambukizi hayo.

Daktari wa kibinafsi wa Odinga David Oluoch-Olunya Alhamisi usiku alithibitisha kuwa kiongozi huyo wa chama cha ODM aliambukizwa Covid-19 lakini anazidi kupata nafuu huku akipokea matibabu katika Nairobi Hospital.

Kutokana na maambukizi hayo, Waziri mkuu huyo wa zamani atajitenga baada ya kukubaliana na madaktari wake.

“Ningependa kuchukua fursa hii kusisitiza kuwa Covid-19 ipo, na tunapaswa kuzingatia masharti yaliyowekwa na serikali, wanasayansi na wataalam wa afya,”alisema Raila.

Wizara ya afya tayari imetangaza kuwa nchi hii inakabiliana na wimbi la tatu la maambukizi ya Covid-19.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *