Categories
Kimataifa

WHO yaibua wasi wasi kuhusu kuyumba kwa vita dhidi ya Malaria Barani Afrika

Shirika la Afya Duniani, WHO, limeonya kuwa upungufu wa fedha unatishia kuathiri juhudi za kukomesha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria Barani Afrika.

Ufadhili wa kukabiliana na Malaria duniani ulifikia dola bilioni tatu mwaka uliopita dhidi ya kiwango kilicholengwa cha dola bilioni 5.6.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kwenye taarifa kuwa janga la Korona limeathiri mafanikio yaliopatikana kwa miaka kadhaa kwenye vita dhidi ya Malaria.

Hapa nchini, kuna visa vipya milioni 3.5 vya Malaria huku vifo 10,700 vikiripotiwa kila mwaka.

Kwa sasa serikali inatumia asilimia 25 ya fedha zake kufadhili vita dhidi ya malaria huku kiasi kilichosalia kikitolewa na wafadhili wa kigeni.

Kulingana na ripoti ya mwaka huu kuhusu janga la Malaria duniani iliyotolewa wiki iliyopita, vita dhidi ya ugonjwa wa Malaria vinaendelea kuyumba hasa katika nchi za Bara Afrika kama vile Kenya.

Mnamo mwaka wa 2000, viongozi Barani Afrika walitia saini azimio la Abuja ambapo waliahidi kupunguza kwa asilimia 50, vifo vinavyotokana na Malaria katika kipindi cha miaka kumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *