WHO yaanzisha uhamasisho kuhusu aina mpya ya Corona Uingereza

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa linashauriana na maafisa nchini Uingereza kuhusu chamuko la aina mpya ya virusi vya Corona vilivyogunduliwa nchini humo.

Shirika hilo limesema Uingereza imetoa taarifa kuhusu virusi hivyo vilivyobadili umbo ambapo shirika hilo litahamasisha nchi wanachama pamoja na raia.

Aina hiyo mpya ya virusi vinasambaa kwa haraka lakini virusi hivyo sio hatari.

Sehemu kadhaa za Kusini Mashariki mwa Uingereza ukiwemo mji wa London zimewekewa kanuni mpya za kudhibiti msambao wa virusi hivyo.

Uholanzi imesema kuwa itapiga marufuku safari za ndege kutoka Uingereza kufuatia chamuko la virusi hivyo vipya vya Corona ambapo marufuku hiyo itadumishwa kuanzia leo hadi tarehe mosi Januari mwaka ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *