West Brom yampiga teke Slaven Bilic

Slaven Bilic ndiye meneja wa kwanza kwenye ligi kuu Uingereza  kupigwa kalamu msimu  huu, baada ya kutimuliwa na klabu ya West Bromwich Albion Jumatano jioni.

Bilic ameonyeshwa mlango baada ya kurekodi msururu wa matokeo mabovu ambapo ameshinda mechi 1 pekee kati ya 13 za  msimu huu na inadokezwa kuwa Sam Alladyce maarufu kama Big Sam huenda akapokezwa jukumu hilo kiwarani Hawthons.

Bilic alishuhudia timu yake ikilazimisha sare muhimu ugenini mnamo Jumanne  usiku walipotoka sare sare ya 1-1 dhidi ya Manchester City .

Kwenye taarifa kutoka kwa timu hiyo iliyorejea ligini mismu huu , Bilic amepigwa teke pamoja na wasaidizi wake wote  Dean Racunica , Danilo Butorovic na  Julian Dicks .

Alladyce aliye na umri wa miaka 66 anajivuni rekodi nzuri ambapo timu zote 7 alizowahifunza kwenye ligi kuu Uingereza hazijashushwa ngazi .

West Brom maarufu kama Baggies ni ya 19 kwenye ligi kuu Uingereza ikizoa pointi 7 pekee kutokana na mechi 13.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *