Categories
Michezo

Wenyeji Mauritania waadhibiwa na Cameroon AFCON U 20

Wenyeji Mauritania waliishia kujutia kosa moja lililofanywa mwishoni mwa kipindi cha pili na kaumbulia kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Cameroon katika mechi ya ufunguzi kuwania kombe la AFCON kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 katika uwanja wa Olimpiki mjini   Nouakchott Jumapili usiku.

Junior Sunday Jang  aliwafungia Cameroon bao la pekee na la ushindi katika   dakika ya 81  akitumia makosa ya mlinzi wa Mauritania aliyepiga pasi kwa kipa wake lakini ikawa fupi na kutwaliwa na mshambulizi huyo aliyepachika bao .

Mauritania wanaoshiriki kwa mara ya w kwanza walidhihirisha mchezo wa hali ya juu huku wakikosa nafasi za wazi za kupitia kwa Oumar Mbareck na  Adama Diop .

Pasi ya difenda Alioum Moubarak wa Mauritania kwa kipa wake ikikatwa na  Sunday Junior  aliyeipa Cameroon inayoshiriki michuano hiyo kwa mara ya 10 ushindi huo muhimu.

Cameroon watarejea uwanjani tarehe 17 dhidi ya Uganda wakati Mauritania wakichuana na Msumbiji.

Mashindano hayo yanayoshirikisha mataifa 12 yataingia siku ya pili Jumatatu kwa jumla ya mikwangurano  mitatu,Uganda wakifungau kazi dhidi ya Musmbiji kuanzia saa kumi alasiri katika kundi A ,kabla ya Burkina Faso kukabiliana na Tunisia saa moja usiku kundini B nao  Namibia wamenyane na Jamhuri ya Afrika ya kati.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *