Waziri wa zamani Simeon Nyachae aaga dunia

Waziri wa zamani Simeon Nyachae ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 88.

Kulingana na taarifa ya familia yake, Nyachae amefariki Jumatatu katika Hospitali ya Nairobi alipokuwa akipokea matibabu.

Alihudumu kama Mbunge wa eneo la Nyaribari Chache kwa miaka 15.

Aidha, alihudumu kama Waziri wa Fedha na Kilimo wakati wa utawala wa Hayati Daniel Arap Moi, miongoni mwa nyadhifa nyenginezo.

Nyachae aliwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2002 lakini akaibuka nafasi ya tatu kwenye matokeo ambayo Rais Mstaafu Mwai Kibaki aliibuka mshindi.

Mbali na siasa na uongozi serikalini, Nyachae pia alikuwa mwanabiashara tajika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *