Waziri wa barabara kaunti ya Narok afariki dunia

Waziri wa barabara na huduma za jamii katika serikali ya kaunti ya Narok, John Marindany ameaga dunia.

Marindany ambaye aliwahi kuhudumu katika wizara mbali mbali katika serikali ya gavana Samuel Tunai, alifariki Jumanne jioni baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Gavana Tunai amesema kifo cha Marindany ni pigo kwa serikali yake kwani alijitolea katika kazi yake.

Gavana huyo amefariji familia ya Marindany, watoto na wakazi wa wadi ya Angata Barrikoi ambapo anatoka.

Marehemu Marindany amehudumu katika idara mbali mbali kama waziri miongoni mwao kilimo ufugaji na uvuvi, elimu , vijana na michezo, afya na usafi na barabara na utumishi wa umma, ambapo alikuwa akihudumu hadi kifo chake.

Haijabainika wazi kilichosababisha kifo chake ambacho kilitokea katika hospitali ya Nairobi women.

Marinday amefariki dunia akiwa naumri wa miaka 52.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *