Wavuvi wa Lamu kupewa kadi za kielektroniki za ‘Mvuvi’

Takribani wavuvi elfu tano kutoka Kaunti ya Lamu watapewa kadi za Mvuvi kuanzia mwezi ujao katika hatua inayokusudiwa kuiwezesha serikaki ya kitaifa kuboresha usalama katika eneo lake la bahari.

Kuanzia mwezi ujao, wavuvi watapewa kadi hizo kupitia kituo cha Huduma kilichoko kisiwani Lamu.

Kadi ya Mvuvi itakuwa na maelezo ya kiektroniki kumhusu kila mvuvi wa humu nchini.

Ni mradi ambao umefadhiliwa na mashirika ya kijamii, yakiwemo Kiunga Youth Bunge, Search for Common Grounds na The ICT Authority Together kwa kushirikiana na taasisi za usalama za serikali ya kitaifa na ile ya kaunti.

Kamishna wa Kaunti ya Lamu Irungu Macharia amesema mpango huo utawezesha wavuvi kuendesha shughuli zao bila kuingiliwa.

Macharia amesema hayo wakati wa kongamano la wadau ambalo liliandaliwa kwenye kisiwa cha Lamu kuhusu uzinduzi wa mpango wa kadi za Mvuvi.

Kamishna huyo amesema ufanisi wa mpango huo utawezesha kuzinduliwa kwa mipango sawia katika Kaunti za Kilifi, Kwale na Mombasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *