Watu watatu wakamatwa na maafisa wa DCI kwa kupokea pesa kwa njia haramu

Maafisa kutoka idara ya upelelezi-DCI wamewatia mbaroni  washukiwa watatu wanaodaiwa walimshika mateka na kumtorosha mkurugenzi wa kampuni ya Hi-Tech Enterprise wakijifanya kuwa maafisa  kutoka tume ya madili na kupambana na ufisadi-EACC na halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini-KRA.

Washukiwa hao waliitisha hongo ya shilingi milioni mbili kutoka kwa jamaa huyo ili waachane na uchunguzi kuhusu ukwepaji wa kulipa kodi na kampuni hiyo.

Kwenye taarifa iliopachikwa kwenye ukurasa wa Twitter,maafisa hao wa DCI walisema washukiwa hao,Godwins Otieno Agutu,Alex Mutu Mutuku na Ken Kichovi Kimathi pamoja na wenzao ambao hawajakamatwa ambao wangali wanayatumia magari mawili aina ya Prado yenye namba za usajili GKB 070B na KCY 280Q,waliingia kwenye afisi za jamaa huyo Jiini Nairobi  tarehe 26 mwezi septemba na kuondoka na kipakatalishi chake.

Hatimaye waliitisha hongo ya shilingi milioni 2,lakini aliposhindwa kutoa hongo hiyo walimlazimisha kuingia kwenye gari lao na kuelekea hadi jumba la Lutheran kwenye barabara ya Nyerere.

Washukiwa hao walimlazimisha jamaa huyo kuarifu familia yake ili kupata pesa hizo, lakini walifanikiwa tu kukusanya shilingi 500,000 ambapo walimpeleka hadi nyumbani kwake mtaani Nairobi West baada ya  kuchukua pesa hizo.

Wakati wa uchunguzi,maafisa hao wa DCI walisema waliwanasa washukwa hao katika jumba la Lutheran.

Aidha walibainisha kuwa gari walilokuwa wakitumia lenye usajili wa namba GKB 070B aina ya Landrover Discovery lilikuwa la idara ya mahakama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *