Categories
Michezo

Watu elfu 6 kuingia uwanjani wakati wa Kip Keino Classic Oktoba 3

Serikali inatarajiwa kuwaruhusu mashabiki wapatao elfu 6  kuingia ndani ya uwanja wa taifa wa Nyayo kushuhudia mashindano ya Kip Keino Classic world continental tour tarehe 3 mwezi ujao.

Kulingana na Rais wa chama cha raidha Kenya Jenerali mstaafu Jackson Tuwei wanasubiri idhini kutoka kwa wizara ya michezo ili kuanza kuuza tiketi hizo huku wale tu watakaokuwa na tiketi wakiruhusiwa uwanjani.

‘’tumetuma maombi kwa serikali iliruhusu tuwe na mashabiki elfu uwanjani ambao wataboresha mashindano hayo’’

Tuwei amesema haya leo katika uzinduzi wa mashindano ya Kip Keino  Classic huku akifichua kuwa shughuli ya ujenzi wa uwanja inakaribia asilimia  98.

Kwa upande wake waziri wa michezo Dr Amina Mohammed ameahidi kuwa Kenya itaandaa mashindano ya kufana baada ya kuandaa mashindano ya dunia kwa chipukizi wasiozid umri wa miaka 18 mwaka 2018 kwa  njia ya kufana na kuwavutia mashabiki wengi.

Waziri wa Michezo Dr Amina Mohammed akiwa na mwenyekiti wa chama cha riadha Kenya Jackson Tuwei,Dr Kipchoge Keino,Baranaba Kori na wanariadha katika uzinduzi wa mashindano ya Kipkeino classic

Aliyekuwa rais wa kamati ya olimpiki nchini Nock Dr Kipchoge Keino ambaye mashindano hayo yemepewa jina lake,amesema ni fursa mwafaka kwa Kenya kuandaa mashindano ya kwanza  ya kimataifa barani Afrika tangu michezo ifungwe mwezi Machi kutokana na janga la covid 19.

Mashindano hayo yataandaliwa tarehe 3 mwezi ujao  huku yakiwa ya vitengo vitatu,mashindano ya kitaifa ,mashindano ya Discretionary na yale ya kimataifa .

Mashindano ya kimataifa yatashirikisha mbio za mita 200 na mita 3000 kuruka maji na viunzi na mashindano ya  ndani ya uwanja  ya Tripple jump na Hammer throw.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *