Watu elfu 10 kuruhusiwa Kip Keino Classic

Mashabiki wasiozidi 10,000 wataruhisiwa kuingia uwanja wa taifa wa Nyayo kushuhudia mashindano ya Kip Keino Classic Oktoba 3 .

Kulingana na mkurugenzi wa mashindnao hayo Barnaba Korir matayarisho yote yamekamilika huku wanariadha wa kimataifa wakitarajiwa kuwasili nchini kaunzia kesho.

‘’Serikali imeruhusu watu elfu 10 kuingia uwanjani,tutazingatia masharti yote ya afya ,matayarisho yamekamilika na maafisa wa shirikisho la riadha ulimwenguni watawasili kuanzia leo’’

Jumla ya wanariadha 150 kutoka nchini na kimataifa watashiriki mashindano hayo ambayo ndio makubwa ya kwanza kuandaliwa barani Afrika mwaka huu.

Uwanja wa Nyayo utakaoandaa mashindano ya Kip Keino Classic

Mashindano hayo yalipangwa kuandaliwa mapema mwezi Mei mwaka huu, lakini yakaahirishwa kutokana na janga la Covid 19.

Uwanja wa Nyayo ulifunguliwa rasmi na Rais Uhuru Kenyatta jumamosi iliyopita .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *