Watu 497 zaidi waambukizwa Corona huku wagonjwa 16 wakiaga dunia

Watu 497 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona baada ya sampuli 4,888 kupimwa katika masaa 24 yaliyopita na kufikisha 46,144, jumla ya maambukizi humu nchini.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara ya Afya, 471 kati ya visa hivyo vipya ni Wakenya na 26 ni raia wa kigeni.

Visa 295 ni vya wanaume na 202 ni vya wanawake, kuanzia umri wa mwaka mmoja hadi miaka 88.

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa visa 227 ikifuatwa na Machakos kwa visa 64, Mombasa 51, Uasin Gishu 37, Laikipia 28, Busia 19, Kajiado 11, Embu 10, Nakuru 9, Wajir 7, Kiambu 6, Kilifi 6, Kisumu 4, Nyeri 4, Makueni 3, Elgeyo Marakwet 2, Meru 2, Kisii 2, Turkana 2, Narok 1, Homabay 1 na Kakamega 1.

Wakati uo huo, wagonjwa 238 wamethibitishwa kupona, 170 kati yao kutoka kwa mpango wa kuhudumiwa nyumbani na 68 kutoka kwa vituo vya afya. Hii imefikisha idadi jumla ya waliopona hadi 32,760.

Hata hivyo, wagonjwa 16 zaidi wameaga dunia kutokana na virusi hivyo na kufikisha jumla ya waliofariki hadi 858.

Kulingana na taarifa hiyo pia, wagonjwa 1,189 wanapokea matibabu katika vituo mbali mbali vya afya humu nchini nao 2,661 wako kwenye mpango wa kuhudumiwa nyumbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *