Categories
Habari

Watu 410 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Kenya imenakili visa 410 vipya vya virusi vya Covid-19 baada ya kupimwa kwa sampuli 7,180 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Hii imefikisha idadi jumla ya maambukizi ya Corona hapa nchini kuwa 105,467.

Kati ya visa hivyo vipya, watu 368 walikuwa wakenya huku watu 42 wakiwa raia wa kigeni.

Mgonjwa mchanga zaidi ana umri wa mwaka mmoja huku mgonjwa mkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 83.

Wagonjwa 24 walipata nafuu ambapo 11 walikuwa wakitibiwa nyumbani huku 13 wakiruhusiwa kutoka katika hospitali mbalimbali humu nchini.

Idadi jumla ya waliopona virusi vya Covid-19 hapa nchini sasa ni watu 86,521.

Hata hivyo wagonjwa sita waliaga dunia na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kutokana na  Covid-19 hapa nchini kuwa watu 1,853.

Kwa sasa wagonjwa 342 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini huku wagonjwa 1,420 wakitibiwa nyumbani.

Wagonjwa 61 wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, ambapo 25 Kati yao wanatumia vipumulio na 27 wakitumia hewa ya ziada ya oxygen huku wagonjwa 9 wakiwa bado wanachunguzwa.

Kaunti ya Nairobi iliongoza baada ya kunakili visa 254 huku ikifuatwa na kaunti ya Mombasa ambayo iliandikisha visa 27.

Kaunti ya Migori iliandikisha visa 24 huku kaunti ya Kiambu ikinakili visa 22.

Nakuru ilikuwa na visa 15, Turkana 13, Machakos 8, Kericho na Uasin Gishu visa 6 kila kaunti.

Kajiado na Taita Taveta zilinakili visa 5 kila moja huku Kilifi,Meru na Nyeri ziliandikisha visa 4 Kila kaunti.

Busia, Kakamega, Kisumu na  Kwale zilinakili visa 2 Kila kaunti huku  Makueni, Kirinyaga, Kitui,Wajir na  Bungoma zikirekodi kisa kimoja kila kaunti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *