Watu 21 zaidi wafariki kutokana na Covid-19 huku visa 1,008 vipya vikinakiliwa hapa nchini

Wizara ya afya imethibitisha visa 1,008 vipya vya Covid-19 katika muda wa saa 24 zilizopita na kufikisha idadi jumla ya virusi hivyo humu nchini kuwa 59,595.

Visa hivyo vipya vilinakiliwa baada ya kupimwa kwa sampuli 6,038. Hadi kufikia sasa wizara ya afya imefanyia uchunguzi idadi jumla ya sampuli 723,210.

Kati ya visa hivyo vipya, 972 ni wakenya ilhali 36 ni raia wa kigeni. Mchanga Zaidi ana umri wa miezi miwli ilhali mkongwe Zaidi ana miaka 95.  616 ni wa kiume huku 392 wakiwa wa kike.

Kulingana na waziri wa afya Mutahi Kagwe, wagonjwa 802 wamepona virusi hivyo,679 kutoka mpango wa utunzaji wa nyumbani huku 123 wakiruhusiwa kuondoka katika vituo mbali mbali vya afya.

Idadi jumla ya wagonjwa waliothibitishwa kupona virusi vya Covid-19 hapa nchini sasa ni 39,193.

Wagonjwa 1,262 wangali wamelazwa katika hospitali mbali mbali hapa nchini huku 5,189 wakiwekwa katika mpango wa kuwahudumia wagonjwa nyumbani.

Wagonjwa 62 wako katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU, 26 katika mitambo ya kuwasaidia kupumua na 31 wakiwekwa hewa ya ziada.

Wakati uo huo idadi ya maafa kutokana na covid-19 inaendelea kuongezeka huku watu 21 zaidi wakifariki katika saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya vifo vinavyotokana na virusi vya Corona hapa nchini sasa ni 1,072.

Kaunti ya Nairobi iliendelea kunakili idadi kubwa ya maambukizi mapya huku ikinakili visa vipya 417, Mombasa 87, Kiambu 51, Kajiado 48, Nakuru 35, Kisumu 32, Kakamega 32, Trans Nzoia 26, Kilifi 24, Nyandarua 23, Kericho 23, Uasin Gishu 23, Nyamira 21 and Machakos 20.

Kaunti ya Migori iliandikisha visa 16, Nyeri 15, Murang’a 14, Turkana 13,Siaya 10, Mandera 9, Busia 8, Meru 7, Kisii 7, West Pokot 6, Tharaka Nithi 6, Makueni 6, Homabay 6, Elgeyo Marakwet 5, Embu 4 na Nandi visa 3.

Kaunti za Kirinyaga, Bometna  Bungoma zilinakili visa 2 kila moja huku  Samburu, Baringo,Wajir, Kwale na Taita Taveta zikinakilia kisa kimoja kila moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *