Watu 190 zaidi waambukizwa Covid-19 humu nchini

Kenya imenakili visa 190 vipya vya maambukizi ya virusi vya Covid-19 na kufanya idadi jumla ya maambukizi humu nchini kuwa 35,793.

Visa hivyo vilipatikana baada ya kupimwa kwa sampuli  4,609 katika muda wa saa  24 zilizopita, na kujumwisha idadi ya watu waliopimwa virusi hivyo humu nchini kufikia 490,445. 

Taarifa kutoka wizara ya afya imesema kati ya visa hivyo, watu 182 ni Wakenya na wanane ni raia wa kigeni.

Mwathiriwa mwenye umri mdogo alikuwa na mwaka mmoja huku mkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 85.

Wagonjwa 395 wamepata nafuu katika muda wa saa 24 zilizopita na kufikisha idadi yao kuwa watu  22,047.

Kati ya waliopata nafuu, 116 walikuwa wakihudumiwa nyumbani na 279 walikuwa katika hospitali mbali-mbali za humu nchini.

Hata hivyo wagonjwa wanne zaidi waliaga dunia na kufikisha idadi vifo kuwa 616.

Kaunti ya  Nairobi iliongoza kwa visa vipya vya maambukizi baada ya kuripoti visa vipya 65, ikifuatwa na Kaunti ya Kitui kwa visa 27 nayo Mombasa imekumbwa na visa 16.

Uasin Gishu ilinakili visa 13, Embu 10, Kisii 9, Garissa 6, Kajiado 6, Kiambu 6, Machakos 4, Nakuru 4, Meru 4, Kericho14, Narok 4, Kisumu 2, Trans Nzoia 2, Bomet 2, Busia 2 huku  Murang’a, Bungoma, Kakamega na Kilifi  zikinakili kisa kimoja kila moja.

Visa vya Nairobi vilipatikana Roysambu ikiwa na visa 14, Dagoretti Kaskazini na  Langata visa 8 kila koja,Embakasi mashariki na Starehe visa 5 kila moja, Embakasi kusini na Westlands visa 4 kila moja, Embakasi magharibi  (3), Dagoretti kusini,  Embakasi ya kati, Kamukunji, Kibra na Makadara visa viwili kila moja,Embakasi kaskazini, Kasarani, Mathare na Ruaraka kisa kimoja kila moja.

Katika kaunti ya  Embu visa vyote vilipatikana Manyatta, huku visa 9 vya kisii vikinakiliwa  Kitutu Chache kusini visa 6 na Bonchari 3.

Visa sita vya Garissa vilinakiliwa Garissa mjini huku visa vya kajiado vikipatikana Kajiado kaskazini.

Kaunti ya Kiambu ilipata visa vyake  Thika na visa 4, huku Kiambu mjini na Ruiru zikiwa na kisa kimoja kila moja. katika kaunti ya Machakos,visa vyote vinne vilipatikana machakos mjini.

Kaunti ya  Nakuru ilinakili visa vyake  Nakuru mashariki visa 2 nazo  Gilgil na Nakuru kaskazini zikiwa kisa kimoja kila moja,.

Visa vinne vya Meru vilitoka Buuri, Imenti ya kati, Tigania mashariki na Tigania magharibi zikiwa a kisa kimoja kila moja.

Nayo kericho ilipata visa vyake vinne  Belgut visa 3 na  Ainamoi kisa kimoja.

Visa vyote vya  Narok  vilitoka Narok kaskazini. Huku visa vya Trans Nzoia vikinakiliwa Kiminini.

Kaunti ya Bomet ilitoa visa vyake  Bomet ya mashariki  huku visa viwili vya Busia vikiandikishwa Teso kaskazini.

Kaunti ya Murang’a, ilinakili visa vya covid-19 Maragua, nacho kisa kimoja cha Bungoma kikinakiliwa  Kimilili.

Kisa cha Kakamega kilipatikana Ikolomani, huku cha  Kilifi kikiandikishwa Kaloleni.

Katika kaunti ya Kitui, visa 27 vilipatikana Kitui Magharibi visa  (24), Mwingi ya kati (2) na kitui Mashambani kisa kimoja.

Kaunti ya Uasin Gishu ilinakili visa vyake 13 kutoka Ainabkoivisa  (6), Soy (3), Kapseret (2), Moiben na Turbo zikiwa na kisa kimoja kila moja.

Na kaunti ya Mombasa ilipata visa vyake 16 kutoka Jomvu visa (6), Mvita (4) huku Changamwe na Kisauni zikiwa na visa vitatu kila moja.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *