Watu 18 zaidi wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Watu 18 wamefariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19 katika muda wa saa 24 zilizopita kwenye taarifa ya hivi punde, ambapo visa 629 zaidi vya maambukizi ugonjwa huo vimeripotiwa.

Hii ni kutokana na sampuli 5,823 zilizopimwa katika muda huo. Kati ya visa hivyo vipya vya maambukizi, 612 ni vya Wakenya na ilhali 17 ni vya raia wa kigeni.

Kulingana na taarifa hiyo ya wizara ya afya,mgonjwa mchanga zaidi ni mtoto wa mwaka mmoja huku yule mkongwe akiwa na umri wa miaka 92.

Jumla ya visa vya maambukizi humu nchini sasa vimefikia 153,523 ilhali jumla ya sampuli zilizopimwa ni 1,611,679 huku kiwango cha maambukizi kikiwa asilimia 10.8.

Wagonjwa 1,560 wamepona Covid-19 katika muda wa saa 24 zilizopita ambapo 1,358 walikuwa katika mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani na 202 waliruhusiwa kuondoka katika vituo mbali mbali vya afya kote nchini..

Idadi jumla ya waliopona Covid-19 hapa nchini sasa ni watu 103,838 ambapo 75,650 kutoka mpango wa kuwahudumia wagonjwa nyumbani na 28,188 ni kutoka taasisi mbali mbali za afya.

Ugonjwa huo ungali unawaathiri wanaume zaidi kuliko wanawake ambapo kati ya visa hivi vipya 358 ni vya wanaumr ikilinganishwa na visa 271 vya wanawake.

Kaunti ya Nairobi ingali inaongoza kwa visa 201 ikifuatiwa na Kericho kwa visa 32 ,Nakuru 37, Kiambu 36, Machakos31, Garrisa 25 na Kilifi 22.

kaunti zenye visa vichache zaidi vya maambukizi ni Makueni na Narok, ambavyo vina vina visa vitatu kila moja. Murangá visa viwili huku Pokot-magharibi,Elgeyo Marakwet, Kisii, Kwale na Migori zina kisa kimoja kila kaunti.

Taarifa ya wizara ya afya pia inasema watu 721,509 wamepokea chanjo kote nchini huku Nairobi ikiwa na idadi kubwa zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *