Watu 15 wakamatwa Afrika kusini kwa madai ya ufisadi yanayohusiana na mazishi ya Mandela

Polisi nchini Afrika kusini wamewakamata watu 15 kwa madai ya ufisadi yanayohusiana na mazishi ya aliyekuwa Rais, Nelson mandela mwaka wa 2013.

Waliokamatwa ni pamoja na waziri wa afya wa jimbo la Eastern Cape, Sindiswa Gomba, wafanyibiashara kadhaa na wabunge wengine kutoka chama tawala cha African National Congress.

Miongoni mwao ni mwenyekiti wa kanda, Pumlani Mkolo, aliyekuwa meya wa mji wa Buffalo, Zukiswa Ncitha na spika wa baraza la jiji Luleka Simon-Ndzele.

Watu hao 15 ambao wameachiliwa kwa dhamana hadi mwezi ujao, wameshtakiwa kwa ufisadi na magendo ya fedha za kiasi cha dolla laki saba.

Viongozi wa mashtaka wanasema walifanya madai ya kilaghai ya uchukuzi wa waombelezaji na maeneo yaliotumiwa katika mji wa East London kwa ibada za ukumbusho za aliyekuwa Rais wa kwanza Mwafrika nchini Afrika kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *