Watu 130 zaidi waambukizwa ugonjwa wa COVID-19

Wizara ya Afya humu nchini imetangaza visa vipya 130 vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19, kutokana na sampuli 4,918 zilizopimwa masaa 24 yaliyopita.

Visa hivyo vimeongeza idadi ya maambukizi hadi kufikia 100,323 kutokana na jumla ya sampuli 1,167,409 zilizopimwa kufikia sasa.

Visa 115 ni vya Wakenya huku 15 vikiwa vya raia wa kigeni, wanaume 88 na wanawake 42, wote wa kati ya umri wa miezi minne hadi miaka 88.

Kaunti ya Nairobi imenakili visa 66, Taita Taveta 18, Mombasa 9, Nakuru 6, Narok 6, Siaya 4, Uasin Gishu 4, Kiambu 4, Kisii 4, Kilifi 2, Kisumu 1, Bungoma 1, Busia 1, Kajiado 1, Kakamega 1, Nyamira 1 na Nyandarua 1.

Wizara ya Afya pia imethibitisha kupona kwa wagonjwa 66 na kuifanya idadi jumla ya waliopona humu nchini kufikia 83,691.

Kati ya hao waliopona, 42 walikuwa wakitibiwa nyumbani ilhali 24 walikuwa wakitibiwa hospitalini.

Hata hivyo mmgonjwa mmoja zaidi wamethibitishwa kuaga dunia kutokana na ugonjwa huo na kufikisha jumla ya maafa hadi 1,751.

Kufikia sasa, kuna jumla ya wagonjwa 489 wanaohudumiwa katika vituo mbali mbali vya afya humu nchini huku wengine 1,353 wakiwa katika mpango wa uangalizi wa nyumbani.

Wagonjwa 28 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi, 14 kati yao wakitumia vipumuzi ilhali 13 wanapokea hewa ya oksijeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *