Watu 1,185 zaidi wameambukizwa Covid-19 huku 17 wakifariki hapa nchini

Nchi hii imenakili visa 1,185 vipya vya maambukizi ya Covid-19 huku watu 17 zaidi wakifariki kutokana na makali ya virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya watu walioambukizwa virusi vya corona humu nchini sasa ni 53,797.

Jumla ya waliofariki kutokana na ugonjwa huo hapa nchini sasa ni  981 huku visa hivyo vipya vilithibitishwa baada ya sampuli 9,851 kupimwa na kufikisha 687,000 jumla ya sampuli zilizopimwa hapa nchinio.

Akiongea wakati wa vipasho vya kila siku kuhusu hali ya virusi vya corona hapa nchini, waziri wa afya  Mutahi Kagwe alisema wagonjwa 1,119 kwa sasa wamelazwa hospitalini.

Wagonjwa wengine 4,440 wako kwenye mpango wa kuwahudumiwa wagonjwa wa Covid 19 nyumbani.

Kagwe alisema wagonjwa  41 wamelazwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi , huku 26 kati yao wakitumia vipumuzi na 15 wakitumia hewa ya oksijeni ya ziada.

Mwathiriwa wa umri mdogo zaidi ana miezi 11 na wa umri mkubwa zaidi ana miaka 93.

Kagwe alisema kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa visa vya maambukizi huku ikiwa imenakili visa 25,226.

Aliongeza kuwa watu 257 wamepona ambapo , 203 kati yao walikuwa wakihudumiwa nyumbani na 54 wameruhusiwa kuondoka hospitalini.

Amewahimiza wakaenya kuzingatia kanuni za kuzuia maambukizi ya corona zilizotolewa na wizara ya afya huku visa vya maambukizi vikiendelea kuongezeka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *