Watu 10 wafariki hapa nchini kutokana na Covid-19

Wagonjwa kumi wamefariki kutokana na virusi vya Covid-19 katika muda wa saa 24 zilizopita na kufikisha idadi jumla ya waliofariki kutokana na virusi hivyo hapa nchini kuwa watu 1,837. 

Hata hivyo idadi jumla ya waliopata nafuu baada ya kupona covid-19 sasa ni watu 85,665 baada ya wagonjwa 39 kupona. Katika muda wa saa 24 zilizopita.

Wagonjwa 36 waliruhusiwa kuondoka katika hospitali mbalimbali nchini huku watatu wakipona kutoka mpango wa kuwatunza wagonjwa nyumbani.

Haya yanajiri huku nchi hii likinakili visa vipya 194 vya virusi hivyo baada ya kupimwa kwa sampuli 3,935 katika muda wa saa 24 zilizopita

Haya ni kwa mujibu wa taarifa kutoka wizara ya afya kuhusu hali ya virusi vya corona nchini.

Idadi jumla ya visa vya maambukizi vilivyodhibitishwa nchini kufikia sasa ni watu 104,500. 

Katika visa vilivyodhibitishwa, watu 146 ni raia wa Kenya huku 48 wakiwa raia wa kigeni. Wagonjwa 108 ni wanaume huku 86 wakiwa wanawake.

Mgonjwa mchanga zaidi alikuwa na umri wa miaka sita huku mkongwe zaidi akiwa na umri wa miaka 95. 

Kaunti ya Nairobi ingali inaongoza kwa visa 32 ikifuatwa na kaunti ya Kiambu kwa visa tisa.

Kaunti ya Meru ilikuwa na visa saba huku Kisumu na Kilifi zikiandikisha visa sita kilamoja.

Kaunti ya Laikipia ilinakili visa vitano huku kaunti ya Mombasa na Kajiado zikinakili visa vinne kila moja.

Kaunti za Nakuru, Turkana, Uasin Gishu na Machakos zilikuwa na visa vitatu kila moja.

Wagonjwa 565 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi. Wagonjwa sita wanafanyiwa uchunguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *