Washukiwa watano wakamatwa na mali ya wizi Jijini Nairobi

Maafisa wa polisi jijini Nairobi wamepata mali ya thamani isiyojulikana iliyokuwa imeibwa na kuwakamata washukiwa watano wanaominika kuhusika kwenye visa kadhaa vya wizi wa kimabavu jijini Nairobi.

Kamanda wa polisi wa eneo hilo Rashid Yakub alisema kuwa kwenye operesheni iliyotekelezwa jijini katika muda wa siku nane zilizopita, maafisa wa polisi walipata vipakatalishi 250, simu 84 za rununu za aina mbalimbali, vipuri vya magari, sare bandia za polisi yakiwemo majaketi 77, suruale 64 na njuti 50.

Yakub alisema kuwa maafisa wa polisi waliwakamata washukiwa hao watano waliokuwa sehemu ya kundi ambalo limekuwa likitumia sare bandia za polisi kutekeleza shughuli za kiuhalifu jijini humu.

Washukiwa wawili wamefikishwa mahakamani huku wengine watatu waliotoroka wakati wa msako huo wakitafutwa.

Kuna madai kwamba baadhi ya maafisa katika huduma ya taifa ya polisi huenda wanahusika kwenye njama hiyo.

Wale ambao huenda wameporwa vifaa vyao na wahalifu wametakiwa wazuru makao makuu ya polisi katika eneo la Nairobi ili kuvitambua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *