Washukiwa wa maandamano ya kupinga matokeo ya Urais Tanzania waachiliwa huru

Polisi nchini Tanzania wamewaachilia kwa dhamana viongozi wote wa upinzani waliokamatwa kwa madai ya kufanya maandamano bila kibali.

Wanasiasa hao ni pamoja na mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Freeman Mbowe, na kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.

Wote walishtakiwa kwa makosa ya kuandaa maandamno kinyume cha sheria na makosa ya jinai.

Baadhi ya wanasiasa hao walitiwa nguvuni siku ya jumapili.

Upinzani umeitisha mfululizo wa maandamano ya umma kulalamikia matokeo ya uchaguzi wa urais wa wiki iliopita, ambapo Rais John Pombe Magufuli alishinda kwa aslimia 84 ya kura hizo.

Upinzani umekataa matokeo ya uchaguzi huo na kusema una ushahidi kwamba kulifanyika udanganyifu kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo, polisi wameshtumu wafuasi wa upinzani kwa kuteketeza masoko na vituo vya mafuta ya petrol wakati wa maandamano ambayo yalipangiwa kuanza Jumatatu lakini hayakufanywa.

Siku ya Jumatatu, mgombea urais wa upinzani Tundu Lissu alitiwa nguvuni kwa muda lakini akaachiliwa baadaye kutokana na sababu za kiafya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *