Wanawake wawili wakamatwa wakiwa na silaha hatari Jijini Nairobi

Idara ya Upelelezi kuhusu Uhalifu DCI, na Kitengo cha Polisi wa Kupambana na Ugaidi, jana zilipata silaha na risasi zinazoshukiwa kuingizwa nchini, ili kutumika katika shughuli za ugaidi.

Kupitia ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, idara hiyo ilisema silaha zilizojumuisha bunduki aina ya ya M4, yenye uwezo wa kulenga umbali wa mita 500, zilipatikana kutoka kwa wanawake wawili, Joyce Muthoni Mwihia, na mamake Goretti Mwihia.

Wapelelezi wanasema, wanawake hao wote ambao wanaishi mtaa wa Racecourse Jijini Nairobi, katika eneo la Dagoretti Corner, wana uraia wa nchi mbili.

Wakati wa operesheni hiyo, maafisa wa usalama walipata bastola 4 na bunduki moja ya aina ya Uzi, ambayo inaweza kurusha zaidi ya risasi 600 kwa dakika.

Pia kulipatikana risasi zaidi ya 3,700 za aina tofauti.

Maafisa hao wanawazuilia washukiwa kwa mahojiano zaidi, huku uchunguzi ukiendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *