Wanasiasa watahadharishwa dhidi ya kutoa semi za chuki

Wanasiasa wametahadharishwa dhidi ya kutumia muda wa utekelezaji ripoti ya BBI kutoa semi za uchochezi.

Tume ya uwiano na utangamano wa kitaifa NCIC, imefichua kwamba kwa sasa inawachunguza zaidi ya wanasiasa 40 kwa madai ya kutoa semi za chuki.

Kulingana na kamishna wa tume ya NCIC, Philip Okundi, idara ya mahakama imebainika kuwa kiungo dhaifu kwenye vita dhidi ya semi za chuki akisema kesi nyingi hudumu kwa muda mrefu mahakamani.

Okundi pia alisema sheria hafifu kuhusu semi za chuki inatatiza vita dhidi ya uovu huo.

Kamishna Dorcas Kedogo alisema tume hiyo inawahamasisha Wakenya kuhusu umuhimu wa kujiepusha na semi za chuki.

Alionya kuwa simulizi kuhusu ukinzani wa kitabaka kati ya hustler na mabwanyenye utawagawanya Wakenya kwa misingi ya kitabaka.

Makamishna hao wawili walisema haya huko Kitale katika kaunti ya Trans-Nzoia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *