Wanariadha 6 wanufaika na msaada wa masomo kutoka kwa ANOCA

Bingwa wa jumuiya ya madola katika mita 800 Wyclife Kinyamal,bingwa wa Olimpiki katika mita 3000 kuruka maji na viunzi Consenslus Kipruto ,bingwa wa dunia wa mita 1500,Rodgers Kwemoi aliyeibuka wa 4 katika mita 10,000  mashindano ya dunia ya mwaka 2019 ,bingwa wa kitaifa mita 800 mwaka 2018 Emily Cherotich  na mshindi wa nishani ya shaba ya dunia miat 800 mwaka 2019 Ferguson Rotich wamenufaika na msaada wa masomo wa kima cha shilingi milioni 2 , kutoka kwa kamati za Olimpiki barani Afrika ANOCA.

Wanariadha hao walipokea hundi ya shilingi milioni 2 ambapo kila mmoja atapata  msaada wa masomo wa shilingi laki 4 kutoka kwa Rais wa kamati ya Olimpiki nchini kenya Nock Paul Tergat mapema Jumanne alipoongoza msafara wa viongozi wa maafisa wa NOCK na wale wa timu itakayoshiriki michezo ya Olimpiki kuzuru kambi za mazoezi ya wanariadha wanaojiandaa kwa michezo ya Olimpiki mjini Eldoret.

Tergat akizungumza kwenye hafla hiyo iliyofuatia warsha  iliyohudhuriwa na wanariadha kadhaa ,amesema kuwa atahakisha timu ya kenya inapata maandalizi na matayarisho bora kwa michezo ya Olimpiki ya mwaka huu.

“Tunataka kuwahakikishia kuwa tutafanya kazi kwa pamoja  kama wadau kuhakikisha kuwa wanariadha wote wamejiandaa vyema kwa michezo ya Tokyo .Tunaangalia mbinu zote zilizopo ikiwemo kutoa misaada ya masomo na tunawahimiza wanariadha kutafakari kuhusu maisha yao ya siku za usoni  baada ya kustaafu yanakuwa bora”Akasema Tergat

Rais wa NOCK Paul Tergat akipiga picha na wanariadha watano kati ya 6  waliopokea msaada wa masomo

Kwa upande wake mkurugenzi wa timu ya Kenya ya Olimpiki mwaka huu Barnaba Korir ametoa hakikisho kuwa wanariadha waliofuzu kwa michezo hiyo na wale watakaoshiriki mashindano ya kufuzu ni wale bora pekee ambao wataenda Olimpiki sio tu kushiriki ,bali kutwaa medali.

Maafisa wengine wa NOCK kwenye ziara ya leo ni pamoja na kaimu katibu mkuu  Francis Mutuku na mwakilishi wa wanariadha Humphrey Kayange ambao walijiunga na kocha wa mbio za masafa marefu kutoka kambi ya Kaptagat Patrick Sang.

Bingwa wa Olimpiki katika  mita 5000 Vivian Cheruiyot aliwahimiza wanariadha kutumia vyema pesa wanazopata kupitia riadha haswa  baada ya janga la COVID 19 lililosababisha kusitishwa kwa mashindano yote kote ulimwenguni mwaka uliopita.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *