Wanaoukumbwa na matatizo ya kiakili wahimizwa kutafuta usaidizi

Katibu mwandamizi wa wizara ya utumishi wa umma na masuala aya kijinsia Rachel Shebesh na mwenzake wa wizara ya teknolojia ya habari, ubunifu na masuala ya vijana Nadia Ahmed Abdalla, wameelezea hadharani kuhusu jinsi wanavyokabiliwa na matatizo ya kiakili na kutoa wito kwa wakenya wanaokabiliwa na masaibu sawia kujitokeza kutafuta usaidizi .

Wakihutubia vijana huko Isiolo wakati wa awamu ya eneo la mashariki ya kampeni ya ‘Kenya ni Mimi’ , viongozi hao walisikitika kuwa wakenya wanateseka bila kusema ilhali wanaweza kusaidiwa iwapo watatafuta usaidizi.

Shebesh alisema alipokuwa akihudumu kama mbunge wa kaunti ya Nairobi kati ya mwaka 2012 na 2017, aligundua kuwa alikuwa akikabiliwa na matatizo ya kiakili ambayo aliishi nayo kwa miaka mingi bila kuwa na uwezo wa kuyadhibiti

Viongozi hao walitoa wito kwa vijana kutonyamaza wakiteseka bali watafute usaidizi kutoka kwa watalamu wa utoaji ushauri nasaha na pia watalamu wa matatizo ya kiakili ambao wanapatikana katika hospitali nyingi za umma.

Walisema changamoto za kiakili zimesababisha wakenya wengi kuwa na fikira za kujiua lakini matatizo hayo yanaweza kudhibitiwa iwapo mwathiriwa atatafuta usaidizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *