Wanaopinga usajili wa Huduma Namba awamu ya pili wakosolewa

Kamati ya usalama ya bunge la kitaifa imewakosoa baadhi ya wanasiasa wanaopinga kuzinduliwa kwa awamu ya pili ya usajili wa Huduma Namba.

Kupitia mwenyekiti wake Paul Koinange, kamati hiyo ilisema kuwa wanasiasa wanaopinga usajili huo wanahofia uwajibikaji na vita dhidi ya ufisadi.

Akiongea katika majengo ya bunge,mwenyekiti wa kamati hiyo Paul Koinange aliyepia mbunge wa kiambaa alipuzilia mbali madai ya wanasiasa hao kwamba usajili wa Huduma Namba ni sehemu ya njama kubwa ya wizi wa kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka  2020.

Koinange alikariri kwamba wanaopinga awamu hiyo ya pili ya usajili wa Huduma Number wanavuruga ajenda ya maendeleo ya raia  Uhuru Kenyatta.

Waziri wa usalama wa kitaifa Karanja Kibicho tarehe 16 mwezi huu alidokeza mipango ya kuzindua awamu hiyo ya pili ya usajili wa Huduma Number.  

Alitangaza kwamba awamu hiyo ya pili inawalenga wakenya ambao hawakusajiliwa katika awamu ya kwanza mwaka jana.   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *