Wanamziki wapya kwenye Konde Gang ya Harmonize

Konde Gang kampuni ya muziki inayomilikiwa na mwanamziki Harmonize imewatambulisha wanamuziki wapya ambao wamejiunga nao rasmi leo tarehe 11 mwezi Septemba mwaka 2020.

Harmonize aliwatambulisha Country boy, Cheedy na Killy kuwa wasanii wake hii leo kwenye kikao na wanahabari.

Harmonize pamoja na wanamuziki hao walivaa nguo za kufanana ambazo ni suti nyeusi zenye maua maua ya rangi ya dhahabu kwenye masikio ya koti. Wengine kwenye usimamizi wa Konde Gang walikuwa na suti nyeusi tu.

 

Baada ya kumaliza utambulisho wa wasanii hao wapya Harmonize aliwaelekeza wanahabari kwenye maegesho ya magari ambapo aliwakabidhi Country Boy na Ibra magari aina ya Toyota Crown.

 

 

Harmonize ndiye alikuwa mwanamziki wa kwanza kusajiliwa kwenye kampuni ya Diamond Wasafi wakati ikianza yapata miaka mitano iliyopita.

Alitia saini mkataba wa miaka 15 na Wasafi ila akalazimika kuuvunja mwezi wa tisa mwaka jana kwa kile alichokidai kuwa pato lake jingi kusalia kwenye kampuni naye kulipwa hela kidogo. Baada ya hapo akaanzisha Konde Gang.

Msanii wa kwanza kugura Wasafi ni Rich Mavoko aliyefanya vile mwaka 2018.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *