Wanamichezo 107 kusalia kambini Kasarani kujiandaa kwa michezo ya Olimpiki

Wanamichezo zaidi ya 100 walio kwenye kambi ya mazoezi katika uwanja wa Kasarani ,watasalia kambini huku wakijitiyarisha kwa michezo ya Olimpiki makala 32 kuanzia Julai 23 hadi Agosti 8 mwaka huu.

Kulingana na meneja mkuu wa timu ya Kenya Barnaba Korir wanamichezo hao takriban 107 watakuwa wakiishi katika Hoteli ya Kasarani ambako watakuwa wakifanya mazoezi uwanjani na kurejea kwenye mkahawa ingawa hawataruhusiwa kwenda nyumbani.

Korir amesema kambi inaendelea vyema ikiwajumuisha wanariadha wa mbio za masafa mafupi,mabondia,wachezaji voliboli walio katika kambi ya chuo kikuu cha Kenyatta,mhezaji mmoja wa Taekwondo na timu za raga kwa wachezaji 7 upande wanaume na wanawake zinazoshiriki mashindano ya Dubai 7’s kwa sasa.

“Tuko na kama wanamichezo 107 kwenye kambi ya Kasarani wakiwa wanariadha,wachezaji voliboli,mchezaji taekwondo mmoja pamoja na wachezaji wa raga wa timu za wanaume na wanawake zilizo Dubai kwa mashindano ya Dubai 7’s,tunashukuru kuwa wizara ilikubali ombi letu la kuwaacha wanariadha hao wasalie kwenye kambi ile tunaita bubble training wakijiandaa kwa michezo ya olimpiki”

Wanariadha wa mbio za marathon pia wanaendelea na mazoezi kujiandaa kwa michezo ya Olimpiki.

Kenya ilitwaa medali 14 mwaka 2016 mjini Rio De Janeiro Brazil kwa dhahabu 6,fedha 7 na shaba 1.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *