Wanakandarasi kupokea mafunzo ili kuimarisha viwango vya mijengo Nyandarua

Halmashauri ya kitaifa ya ujenzi,NCA, imeshirikiana na serikali ya kaunti ya  Nyandarua kuwapa mafunzo wanakandarasi katika jitihada za kuimarisha viwango vya mijengo  mbalimbali katika eneo hilo.

Afisa mkuu wa maswala ya ujenzi Lawrence Gitau, alisema kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa wanakandarasi waliosajiliwa.

Alisema kuwa watahakikisha wale wanaotekeleza miradi ya ujenzi  katika  eneo hilo wamesajiliwa na wana ufahamu wa kutosha kuhusu maswala mbalimbali katika sekta ya ujenzi huku wakidumisha viwango vya hali ya juu.

Msajili wa halmashauri ya ujenzi katika eneo la kati-kati ya nchi aliye pia meneja wa ubora wa ujenzi, Susan Ruto, alisema kikao hicho cha wadau kiliandaliwa kwa sababu ya ongezeko la mijengo duni katika Kaunti hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *