Wanajeshi washikwa mateka na wagema Mvinyo Kasarani

Tusker Fc wameweka hai matumaini ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya Kenya baada ya kuwashinda wanajeshi Ulinzi Stars goli 1 bila jawabu katika mechi iliyosakatwa Ijumaa alasiri katika uwanja wa Kasarani.

Bao la pekee na la ushindi kwa Tusker lilipachikwa kimiani na Boniface Muchiri katika dakika ya 51 ,ukiwa ushindi wa 11 kwa Tusker Fc msimu huu ,wakirejelea ushindi baada ya kupoteza mechi ya pili dhidi ya Bidco United wiki iliyopita.

Tusker waliopiga mechi 15 wamezoa alama 35 wakifuatwa na KCB kwa pointi 26 wakiwa na mechi 2 mkobani.

Katika mechi nyingne Kariobangi Sharks wamekosa nafasi ya kukwea hadi nambari 2 ligini baada ya kulazimishwa kutoka sare tasa dhidi ya Posta Rangers .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *