Wanajeshi wa Eritrea wajiondoa kutoka eneo la makabiliano la Tigray nchini Ethiopia

Wanajeshi wa Eritrea wameanza kuondoka katika eneo la Tigray nchini Ethiopia baada ya kuiunga mkono serikali katika kukabiliana na waasi wa kundi la Tigray People’s Liberation Front (TPLF).

Marekani, Ujerumani, Ufaransa na mataifa saba yenye ustawi mkubwa duniani G7 siku ya Ijumaa walitoa wito wa kuondolewa kwa wanajeshi hao wa Eritrea na kutekelezwa kwa mchakato wa kisiasa unaokubaliwa na raia wote wa Ethiopia.

Taarifa hiyo pia inapendekeza kubuniwa kwa shughuli ya wazi na inayojumuisha pande zote za kisiasa ambao unakubaliwa na raia wote wa Ethiopia, wakiwemo wale walio Tigray na utakaowezesha kuandaliwa kwa uchaguzi wa haki na mchakato wa kitaifa wa maridhiano.

Wizara ya mashauri ya kigeni ya Ethiopia ilitangaza kujiondoa kwa jeshi hilo lakini ikasema taarifa ya mawaziri wa mashauri ya kigeni wa G7 haikuangazia hatua muhimu ambazo zimechukuliwa kushughulikia mahitaji ya eneo hilo.

Mwezi uliopita, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alikiri kwa mara ya kwanza kwamba wanajeshi wa Eritrea waliingia Tigray wakati wa makabiliano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *