Wanaharakati watabiri ongezeko la mimba za mapema kote nchini

Wanaharakati wa haki za watoto wametoa tahadhari kuhusu ongezeko la mimba za wasichana wadogo kote nchini.

Wanaharakati hao wanasema mwaka uliopita pekee baada ya shule kufungwa kwa muda mrefu kutokana na janga la COVID-19, kuliripotiwa ongezeko kubwa la mimba miongoni mwa wanafunzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Ripples International linalojishughulisha na haki za watoto, Mercy Chidi, anasema mengi yanahitajika kufanywa ili kuhakikisha  jamii  inatekeleza majukumu yake katika kulinda haki za watoto.

Alisema kuwa kuna haja ya serikali na mashirika ya kijamii kukuza ufahamu wa afya ya uzazi katika jamii, akihimiza wazazi na walezi kuongeza umakini katika maswala ya kulinda haki za watoto.

Afisa wa Watoto wa Igembe Kusini, John Mwangi, alisema hali hiyo, hasa katika eneo la Igembe, imekuwa ikiendelea na akina mama wachanga sasa ni nusu ya wanawake wanaojifungua hospitalini.

Mwangi alitaja hali ya kupuuzwa na wazazi na ushawishi wa wenzao kama sababu za visa vingi vya mimba miongoni mwa vijana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *