Wanafunzi wote nchini Uingereza kuchanjwa dhidi ya covid-19

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameahidi kwamba wanafunzi wote huko Uingereza watapewa chanjo yao ya kwanza dhidi ya korona kufikia mwisho wa mwezi Julai.

Zaidi ya watu milioni 17 wamepokea chanjo hiyo tangu shughuli hiyo kuanzishwa nchini humo mwezi Disemba mwaka jana.

Boris amesema anataka mpango huo kuharakishwa.

Amesema chanjo ya mwezi Julai itawasaidia watu wasiojimudu na kusaidia katika kulegeza masharti ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo nchini humo.

Afisa mkuu wa huduma za afya nchini humo Sir Simon Stevens amesema kuna dalili kwamba chanjo iliyotolewa hapo awali imesaidia kupunguza maambukizi na watu kulazwa hospitalini.

Hayo yanajiri huku mji wa Nice nchini Ufaransa ukiwataka watalii kutozuru mji huo kutokana na kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 .

Meya wa Nice ambao ni mji ulioko kusini mwa Ufaransa anataka kuwekwa kwa masharti ya usafiri ili kupunguza idadi ya watalii wanaozuru mji huo akionya huenda visa vya maambujkizi ya korona vikaongezeka.

Kabla ya kuagiza masharti kali za kuzuia msambao wa ugonjwa huo kwa mara ya pili mwezi Novemba,serikali ilifunga baadhi ya mahoteli huko Marseille.

Hata hivyo serikali haikuweka vikwazo hivyo katika maeneo yote kutokana na malalamishi kutoka kwa wanasiasa na wafanyibiashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *