Wanafunzi 68 wa shule ya upili ya wasichana ya Bahati waambukizwa Covid-19

Wanafunzi 68 na walimu watano wa shule ya upili ya wasichana ya Bahati kaunti ya Nakuru wametengwa baada ya kuthibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa COVID 19.

Afisa mkuu wa afya katika kaunti ya Nakuru Dkt. Kariuki Gichuki, kwenye tarifa kwa vyombo vya habari alisema wanafunzi wengine 115 wa shule hiyo wamewekwa karantini.

Dkt. Kariuki alisema mwanafunzi mmoja aliyethibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa COVID 19, alikumbwa na matatizo ya kiafya na anahudumiwa katika wadi ya wagonjwa wa COVID 19 ya hospitali kuu ya mkoa Nakuru.

Aliongeza kusema kwamba kundi la madaktari linachunguza hali ya wanafunzi hao na walimu wao ambao wamewekwa karatini shuleni humo.

Afisa huyo mkuu wa afya amehakikishia umma kwamba idara yake inachunguza hali ya ugonjwa huo katika kaunti hiyo.

Siku ya Jumanne, wanafunzi kadhaa waliripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo katika shule mbali mbali humu nchini.

katika shule ya Kolanya Salvation Army iliyoko kaunti ndogo ya Teso kaskazini katika kaunti ya Busia, wanafunzi wapatao 52 walithibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo.

Siku ya Jumatano shule ya upili ya Voi katika kaunti ya Taita Taveta ilifungwa baada ya walimu watatu kuthibitishwa kuambukizwa COVID-19.

Jijini Nairobi, wanafunzi sita na wafanyakazi watatu wa shule ya upili ya Jamhuri wamethibitihwa kuambukizwa ugonjwa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *