Wamiliki wa vyumba vya wageni Machakos washtumiwa kwa kuvigeuza mabaa

Maafisa wa usalama katika eneo la Mavoko, Kaunti ya Machakos, wameibua wasi wasi kuhusu baadhi ya wamiliki wa vyumba vya wageni ambao wamegeuza biashara zao kuwa ya baa.

Naibu Kamishana wa Kaunti katika eneo la Mavoko Charles Wambugu, anasema wamiliki hao wa vyumba vya wageni wanakiuka pia maagizo ya serikali kwa kuruhusu wateja kuendelea kujiburudisha usiku kucha.

Wamiliki wa biashara hiyo katika mji wa Mlolongo na viunga vyake wamekuwa wakiruhusu wateja kujiburudisha bila kujali maagizo ya serikali.

Kulingana na Wambugu, wafanyibiashara hao walaghai wamekuwa wakiwafungia wateja wao kwenye vyumba vya wageni huku wakiwauzia pombe na miraa, akisema mtaa wa Syokimau na pia miji ya Mlolongo, na Chumvi kwenye barabara kuu ya Mombasa imejulikana kwa uovu huo.

Wambugu anasema maafisa wa usalama hawatalegeza juhudi zao katika kuhakikisha kwamba wakenya wote wanazingatia maagizo ya Wizara ya Afya kwa lengo la kuzuia msambao wa ugonjwa wa COVID-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *