Wamalwa asifia ushirikiano wa serikali na Benki ya dunia katika kuwahudumia wakenya

Waziri wa ugatuzi Eugine Wamalwa amepongeza ushirikiano uliopo  kati ya serikali ya kitaifa na Benki ya Dunia kuhusu uimarishwaji wa huduma kwa wananchi katika kaunti.

Akiongea Ijumaa  Siaya baada ya kuzindua miradi kadhaa,Wamalwa alisema ushirikiano huo katika kipindi cha miaka  miwili iliopita umewezesha kuimarishwa miradi kadhaa ya maendeleo ya thamani ya shilingi milioni 20 katika kaunti.

Alisema fungu kubwa la fedha hizo lilipitia mpango wa kitaifa wa kufadhili ugatuzi na kutumika kuimarishia huduma katika sekta ya afya.

Alitoa mfano wa kituo cha kuwatengea waathiriwa wa ugonjwa wa Covid-19 na chumba cha kujifungulia kina mama cha hospitali ya kaunti ndogo ya Ambira na bustani mbili za starehe mjini Siaya.

Aidha Wamalwa alifungua rasmi makao makuu mapya ya  serikali ya kaunti,yaliojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 75.

Pia alitoa tahadhri dhidi ya safari zisizo za lazima na sherehe kupita kiasi hasa msimu huu wa Disemba ili kuzuia msambao wa ugonjwa wa Covid-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *