Wakuu wa Shule wahimizwa kutekeleza kikamilifu kanuni za COVID-19

Afisa anayesimamia huduma za afya katika kaunti ya Uasin Gishu Everlyne Rotich amewataka wakuu wa shule kutekeleza kikamilifu sheria za Wizara ya Afya zinazonuiwa kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa COVID-19 katika taasisi za elimu.

Ametoa wito huo alipokuwa akihutubia wakuu wa shule kutoka kaunti ndogo za Ainabkoi na Moiben kuhusu uhamasishaji wa mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo katika shule ya upili ya Ngeleltarit.

Bi. Rotich amewataka walimu hao kuhakikisha kuwa watoto kwenye shule zao wanazingatia sheria na kanuni za Wizara ya Afya ili kuzuia kusambaa kwa corona.

“Hakikisheni wanafunzi wenu wanavaa barakoa na kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni kwenye maji yanayotiririka, au watumize vieuzi na kukaa mbali mbali,” akashauri.

Mkurugenzi wa Elimu katika kaunti hiyo Gitonga Mbaka amesema kuwa sheria hizo zina maelezo kamili kuhusu jinsi ya kutekelezwa ili kuafikia malengo yake.

Amesema kuzingatia sheria na kanuni hizo kutahakikisha masomo yanaendelea jinsi yalivyopangwa.

Wiki moja imepita tangu kufunguliwa kwa shule humu nchini baada ya kufungwa kwa takriban miezi saba kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *