Wakimbizi 6 raia wa Sudan Kusini wauawa nchini Uganda

Wakimbizi sita raia wa Sudan Kusini wameuawa, na wengine wanne kujeruhiwa kwenye kambi Madi Okollo,kaskazini mwa Uganda.

Kulingana na msemaji wa polisi katika eneo hilo Josephine Angucia,watu  kumi na watatu tayari wamekamatwa kuhusiana na kisa hicho.

“watu 13 ambao wanashukiwa kuhusika katika mashambulizi hayo dhidi ya wakimbizi hao wametiwa nguvuni na tunawataufa wengine,” alisema Angucia.

Kisa hicho duru zinaarifu kilitokea juzi baada ya wakimbizi ambao idadi yao haijabainishwa kumshambulia mwanamume mmoja ,mkazi wa eneo hilo aliyepatikana akiwalisha mifugo kwenye kambi hiyo.

Maafisa wa usalama katika eneo wangali wanawatafuta washukiwa wengine.

Mwezi Disemba mwaka jana mkimbizi mmoja raia wa Sudan kusini aliuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada katika makabiliano na wenyeji katika kambi moja ya wakimbizi lililoko katika wilaya ya Adjumani.

Kuna takriban wakimbizi million 1.4 nchini Uganda,wengi wao kutoka Sudan Kusini.

Shirika moja la kimataifa la kushughulikia maswala ya wakimbizi, mwaka uliopita lilitoa tahadhari ya kuzuka mzozo katika eneo hilo,kutokana kile lilitaja kuwa   ung’ang’aniaji wa raslimali chache zilizoko katika sehemu hiyo kati ya wakimbizi na wenyeji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *