Wakenya wahimizwa kukumbatia Mradi wa kumiliki nyumba kwa bei nafuu

Wakenya wamehimizwa kukumbatia na kujisali kwa mradi wa kumiliki nyumba za gharama nafuu au affordable housing unaoendeshwa na serikali.

Katibu katika wizara ya ujenzi na maendeleo ya mijini Charles Hinga akizungumza mapema leo na Bonni Musambi na Cynthia Anyango katika Makala ya Zinga kupitia Radio Taifa ,amewarai wakenya kujisali na mradi wa Boma yangu ili kujipatia nyumba zinazojengwa na serikali na kujipunguzia msigo wa kulipa kodi ya nyumba kila mwezi.

Katibu Hinga pia ameusifia mradi wa Kazi mtaani ambao umetoa ajira kwa Zaidi ya vijana elfu 70 haswa waliopoteza kazi kutokana na janga la covid 19.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *