Wakenya kumkabili Cheptegei mashindano ya dunia ya nusu marathon

Wanariadha wa Kenya watakuwa na kazi ya ziada kumdhibiti bingwa wa dunia wa mita 10,000 Joshua Cheptegei katika mashindano ya dunia ya nusu marathon mjini Gdynia  Poland.

Cheptegei atatimka mbio za Jumamosi ikiwa chini ya wiki mbili tangu avunje rekodi ya dunia ya mita 10,000 mjini Valencia Uhispania na pia ni Agosti mwaka huu alipoweka rekodi ya dunia ya mita 5000 mjini Monaco katika mashindano ya diamond league.

Kwa mara ya kwanza Mbio za wanaume zinatarajia bingwa mpya kwani Zersebey Tadese wa Eritrea ba Goefrey Kamworor waliotawazwa mabingwa tangu mwaka 2006 hawatakuwepo nchini Poland Jumamosi hii.

Wanaume wa Kenya walitwaa taji hiyo kwa mara ya mwisho mwaka 2016 .

Kiwott Kandie

Kandie atakuwa mjini Gdynia baada ya kuibuka mshindi mara nne mwaka huu katika mashindano ya mbio za nyika za wanajeshi ,mashidnano ya kitaifa ya mbio za nyika ,kutwaa Ras Al Khaimah Half Marathon mwezi Februari na aliposajili muda bora wa kibinafsi wa dakika  58 na sekunde 58.

Kibiwott      Kandie

Kandie pia alishinda mbio za nusu marathon za Prague kwa dakika 58 na sekunde 38  akioredheshwa wa tano kwa jumla .

Wakenya wengine Benard Kimeli na  Benard Ngeno, wanaojivunia muda bora wa dakika  59 na sekunde  7, watakuwa na  Kandie huku wakishiriki kwa mara ya kwanza .

Ngeno, ni mwanariadha anayekimbia nusu marathon na ametwaa nishani katika mashindano 9 aliyoshiriki.

Mshindi wa nishani ya fedha mwaka 2017 Leonard Barsoton, atakuwepo pia huku akiwa na muda bora wa dakika  59 na sekunde  9 .

Itakuwa mara ya kwanza kwa Barsoton kukimbia mwaka huu.

Upinzani kwa wakenya utatoka kwa Guye Adola wa Ethiopia aliyeshinda Makala ya mwaka 2014 ya mashindano ya dunia ya nusu marathon akimlemea Geofrey  Kamworor  na pia akanyakua taji ya  Delhi Half Marathon.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *