Wakaazi wa Matungu watahadharishwa dhidi ya viongozi walaghai

Mwaniaji  ubunge kwa tiketi ya chama cha ANC kwenye uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Matungu Oscar Peter Nabulindo amewahimiza wakaazi wa Matungu kumchagua kiongozi aliye na maono ya maendeleo badala ya kuhadaiwa na vishawishi vya pesa na ahadi za uongo.

Akizungumza na KBC kwa simu Nabulindo ambaye aliibuka wa pili kwenye uchaguzi wa mwaka 2017 akipoteza kwa marehemu Justus  Murunga ,amesema  analenga kutoa kipa umbele  uboreshaji wa masomo ya wanafunzi kupitia utoaji wa misaada ya masomo maarufu kama bursaries,kuimarisha miundo msingi ,kuongeza ueneaji wa umeme  na kubuni miradi ya kujiendeleza kiuchumi kwa vijana na akina mama.

“Ningependa kwuahimiza wakaazi wa Matungu kwamba wawe na msimamo ,wajue kwamba kura ziko mikononi mwao na wanapopiga kura wanatetea maisha yao,saa hizi kuna watu wanapanga kuwahonga ili wawapigie kura ,kuna watu wanaopanga kununua kura yao au kuwahonga,lakini hao watu wakinunua kura hawajawasaidia ,nawaomba wawe waangalifu“akasema Nabulindo

Nabulindo ambaye ni mfanyibiashara atamenyana na mbunge wa zamani wa eneo hilo David Were kwa tikti ya Odm na Alex Lanya wa UDA pamoja na wagombeaji wa kibinafsi Zaidi ya 6.

Uchaguzi mdogo wa Matungu utaandaliwa tarehe 6 mwezi Machi mwaka huu na kiliachwa wazi kufuatia kifo cha mbunge  Justus Murunga mwishoni mwa mwaka uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *