Wahamiaji 43 wakufamaji katika bahari ya Mediterranean

Ajali mbaya ya meli iliyotokea katika bahari ya Mediterranean kwenye Pwani ya Libya imesababisha vifo vya wahamiaji wapatao  43 waliokuwa wakielekea bara Ulaya.

Hayo yamesemwa na shirika la umoja wa mataifa kuhusu uhamiaji.

Shirika la kimataifa kuhusu uhamiaji (IOM) limesema ajali hiyo iliyotokea Jumanne ndilo janga la kwanza la bahari kutokea mwaka huu na kuhusisha wahamiaji wanaoelekea bara Ulaya kutafuta maisha bora.

Shirika hilo limesema maafisa wa usalama katika mji wa Zuwara nchini Libya waliwanusuru wahamiaji kumi ambao walikuwa raia wa Nigeria,Ghana,Cote d’voire na Gambia .

Limesema waliofariki wote ni wanaume kutoka mataifa ya Afrika Magharibi.

Limesema meli hiyo iliondoka kutoka mji wa  Zawiya siku ya Jumanne na kuzama saa chache baadaye baada ya injini yake kukumbwa na hitilafu.

Libya, ambayo ilitumbukia kwenye lindi la machafuko kufuatia maasi ya mwaka 2011 yaliyomwondoa mamlakani aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Moammar Gadhafi, imeibuka kuwa kituo kikubwa zaidi kinachotumiwa na watu kutoka bara Afrika na nchi za kiarabu wanaotoroka vita na umaskini kuelekea bara Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *