Wagonjwa 13 wafariki kutokana na COVID-19 huku wengine 218 wakiambukizwa

Idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 humu nchini imefika 37,707 Ijumaa.

Hii ni baada ya watu wengine 218 kuthibitishwa kuambukizwa kutokana na upimaji wa sampuli 5,424 saa 24 zilizopita.

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Afya, kati ya visa hivyo vipya, 159 ni vya wanaume na 59 vya wanawake, kutoka umri wa mwaka mmoja hadi miaka 78.

210 ni raia wa Kenya huku 8 wakiwa ni wa mataifa ya kigeni.

Wagonjwa 170 wamethibitishwa kupona kutokana na COVID-19 na kufikisha jumla ya waliopona 24,504.

Kati ya hao, 91 walikuwa wakiuguzwa hospitalini na 79 walikuwa kwenye mpango wa kuwahudumia wagonjwa nyumbani.

Hata hivyo, wagonjwa 13 wameaga dunia na kufikisha 682, idadi ya walioaga dunia kutokana na makali ya ugonjwa huo.

Kaunti ya Nairobi imeongoza kwa kunakili visa 68 ikifuatwa na Kisii 28, Mombasa 21, Kisumu 19, Kiambu 13, Kajiado 11, Busia 10, Machakos 8, Tharaka Nithi 6, Garissa 6, Taita Taveta 5,  Nakuru 4, Uasin Gishu 3, Narok 2, Laikipia 2, Kakamega 2, Kericho 2, nazo Kaunti za Homabay, Murang’a, Bomet, Kilifi, Makueni, Migori, Nyandarua na Nyeri zimenakili kisa kimoja kila moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *